Kane agonganisha vichwa vya mabosi United,City na Chelsea

Baada ya nyota wa klabu ya Tottenham, Harry Kane kutangaza kutaka kuondoka, hatimaye uongozi wa timu hiyo umevunja ukimya na kutoa taarifa juu ya kinachoendelea.

Siku ya Jumatatu Kane aliwaambia wababe hao wa north London kuwa angetamani auzwe haraka iwezekanavyo katika kipindi kijacho cha majira ya joto.

Usajili wa  Kane imekuwa vita kubwa miongoni mwa kablu kubwa Uingereza zikiwemo Manchester City, Manchester United na Chelsea ambazo zimekuwa zikihusishwa.

”Lengo letu ni kumaliza msimu tukiwa imara haraka iwezekanavyo, na hiko ndicho ambacho kila mtu anapaswa kuzingatia.” – Sehemu ya taarifa iliyotolewa na Klabu.

Kane mkataba wake wa sasa na Spurs unamuweka hapo mpaka mwaka 2024, baada ya kusaini kandarasi ya miaka sita mwaka 2018 huku akiwa mchezaji anayelipwa zaidi ndani ya timu hiyo.

Related Articles

Back to top button