Kanumba ndio Muigizaji bora wa Muda wote,R.I.P Legend (Video)

Hapa Tanzania mtu yoyote ukimuuliza muigizaji wake bora wa muda wote atamtaja Steven Kanumba na asilimia kubwa wanaamini baada ya kufariki dunia hata Bongo Movie ilikufa pale pale.
Alikuwa msanii ambaye aliwapa matumaini Watanzania kuhusu kuipeleka Tasnia Kimataifa zaidi maana Movie zake zilishaanza kufika mbali sana.
April 7 mwaka 2012 ndio siku ambayo Tanzania ilipokea Taarifa za kusikitisha zaidi hasa kwa wapenda Movie baada ya kukumbwa na umauti katika hospitali ya Muhimbili.
Alifanya kazi nyingi sana ambazo zimebaki kwenye kumbukumbu ya vichwa vya watu na wengi wanaeleza kuwa hakuna Muigizaji aliyetokea mpaka sasa kukaribia walau kile alichokifanya katika miaka yote ile.
Alifanyikiwa kushinda Tuzo nyingi sana na alikuwa mbunifu na mwenye kubadilika badilika kwenye kazi zake.
Alikuwa kipenzi cha Watanzania na mpaka sasa anaendelea kuishi kwenye mioyobya Watanzania wengi.
Moja ya filamu yake bora ya muda wote ni hii ya Crazy Love ambayo aliigiza kama Professor Kichaa, ilipendwa na watu wengi sana na miongoni mwa waigizaji waliokuwepo hapa ni @shamsaford @hemedyphd na Marehemu GRACE MAPUNDA aliyetutoka siku kadhaa nyuma.
RIP LEGEND ndio neno pekee tunaweza kulitumia kwa sasa, kwenye #Tbt ya leo tumkumbuke MAREHEMU STEVEN KANUMBA, kuna mengi ya kiandika juu yake lakini hayo yanatosha kwa leo.
Unahisi Bongo Movie wa sasa wanatakiwa kufanya nini walau kufikia ubira wa Filamu zake??
Imeandikwa na @el_mando_tz
https://www.instagram.com/reel/DCWJJi9KuTU/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==