BurudaniHabari

Kanye West na Khloé Kardashian, wawashiana moto mitandaoni

Siku ya Jumatano dada wa Kim Kardashian aneyitwa Khloé Kardashian alitoa maoni yake kwenye Instagram kuhusu kauli Kanye West ambapo rapper huyo alizungumza kuhusu aliyekuwafamilia ya Kardashians kunizuia asimuone binti yake Chicago siku ya birthday.

Katika maoni yake, Khloé alizungumzia kuhusu siku ya kuzaliwa ya mpwa wake Chicago – sherehe ya kuzaliwa ya pamoja na binamu Stormi Webster – mapema mwaka huu, ambayo rapper huyo amedai mara kwa mara kwamba Kim Kardashian hakumwalika.

Khoe alianza “Ye unajua nakupenda na sitaki kufanya hivi kwenye mitandao ya kijamii ila WEWE ndio umeyaleta hapa, wewe ni baba wa wapwa zangu na ninajaribu kuwa na heshima lakini naomba UACHANE na Kim na uache kuitumia familia yetu unapotaka kuongea uongo,”

Akibainisha kwamba “kila mtu amechoka” na simulizi ya siku ya kuzaliwa ya binti yake, Khloe aliongeza, “Inatosha tayari. Sote tunajua ukweli.”

“Unajua ni wapi watoto wako wako kila wakati na ulitaka siku tofauti za kuzaliwa. Nimeona meseji zako zote na nimethibitisha hilo. Na ulipobadilisha mawazo yako na kutaka kuhudhuria, ulikuja,” aliandika.

“Kama ulivyojieleza, yeye ndiye anayetunza watoto wako 80%  Khloé aliendelea. “Tafadhali muache yeye na familia yake ili watoto walelewe kwa amani. 🙏🏽 Ninatoka sehemu ya upendo na nina furaha kuendeleza mazungumzo haya faragha ukipenda ”

Kama unavyomjua Kanye West hakukaa kimya alisema kuw ahuo ni uongo na mliktaa kunipa adress ya kwenye kumuona mwanangu ingawa nilifanikiwa alisistiza kuwa  Travis Scott, mpenzi wake na Kylie Jenner, ndiye aliyeshiriki naye eneo la sherehe, akibainisha, “hivyo ndivyo mnavyocheza na baba weusi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents