Promotion

Karibu katika ulimwengu mpya wa Phantom 9 kutoka TECNO

Kauli ya mgeni njoo, mwenyeji apone imedhihirika baada ya ujio wa simu za Phantom kutoka
TECNO mobile. Ni moja kati ya simu pendwa miongoni wa watumiaji wa simu za TECNO toka
2015.

Ni lipi hasa inaifanya matoleo ya Phantom kuiteka soko?

Mara zote Phantom hua inatolewa kila mwaka ikiwa imeshiba specifications na features kali
kuliko! Ilikua ikisemekana kwamba kwakua mwaka jana TECNO hawakutoa toleo la Phantom,
kampuni hiyo ilikua inafanya utafiti na kujipanga kuleta simu ambayo itakua ipo vizuri kwenye
kila sekta.

Tetesi hizo ziligundulika kua ni za kweli baada ya kampuni kuzindua simu hiyo mpya ya
Phantom 9 mwezi huu huko nchini India. Uzinduzi huo ulienda sambamba na kampuni
kutangaza kuongeza mkataba wa ushirikiano wao na klabu kubwa Uingereza ya Manchester
City, pamoja na kubadili kauli mbiu yao kutoka “Experience more” kwenda “Expect More”,
yaani ikimaanisha ‘tarajia zaidi’.

Dhima kuu ya kauli hii ni kuwahakikishia watumiaji wa simu za TECNO juu ya ubora na uimara
zaidi utakaoletwa na kumpuni hii pendwa nchini na kwenye bara kwa ujumla. Kwa sasa,
TECNO inashika nafasi ya 5 Afrika kama kampuni ya simu pendwa.

Nisikuchoshe sana, hakika simu hii imekuja na muundo wa kipekee na mzuri zaidi wa kuvutia.
Kamera tatu za nyuma, kamera ya mbele, kioo kikubwa na kizuri zaidi chenye muundo wa “dot
notch” kwa juu pale katikati.

Tumekua tukiona makampuni mengi ya simu yakiondoa tundu la kuchomeka earphone; lakini
hapa kwenye Phantom 9 TECNO wameona watuachie “earphone jack” ambayo ipo upande wa
chini wa simu hiyo.

We unaona ni jambo gani limekuvutia sana kutoka toleo hili? Endelea kutufuatilia kwa ajili ya
kupata sifa nyingine nyingi pamoja na maelezo ya undani kabisa kuhusiana na TECNO Phantom

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents