Siasa

Karine Jean-Pierre mtu wa kwanza mweusi kuwa Msemaji wa Ikulu ya White House

Rais wa Marekani Joe Biden amemteua Karine Jean-Pierre kuwa msemaji wa Ikulu ya White House, mtu wa kwanza mweusi kushikilia wadhifa huo wa hadhi ya juu.

Katika taarifa, Biden amesifu uzoefu, talanta na uadilifu wa Jean-Pierre akisema kwamba anajivunia kutangaza kuteuliwa kwake kama katibu wa habari wa Ikulu.

Msemaji wa ikulu wa sasa Jen Psaki ameandika kwenye mtandao wake wa Twitter kuwa, Jean-Pierre atakuwa mwanamke wa kwanza mweusi na wa kwanza kutangaza hadharani kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja kuhudumu kama katibu wa habari wa Ikulu ya White House.

Jean-Pierre atachukua nafasi ya Psaki, ambaye alihudumu kama msemaji, kuanzia Mei 13. Jean-Pierre mwenye umri wa miaka 44, aliwahi kufanya kazi kwenye kampeni za rais mstaafu Barack Obama mnamo mwaka 2008 na 2012 na pia kwenye kampeni ya Joe Biden mwaka 2020 kabla ya kujiunga na timu ya rais huyo katika Ikulu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents