Kasampaida arejea Nchini akiwa na Tuzo

Steven Magombeka almaarufu ‘Kasampaida’, mpiga picha maarufu anayefanya kazi na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, ameshinda tuzo ya kuwa miongoni mwa vijana 100 wenye ushawishi mkubwa Afrika. @kasampaida
Kasampaida amewasili usiku wa kuamkia leo Jumanne katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere na kupata mapokezi makubwa, huku mwenyewe akimshukuru Rais Samia kwa kumuamini.
Kasampaida alifanikiwa kuibuka na ushindi wa tuzo hizo zilizotolewa nchini Ghana usiku wa kuamkia juzi ambapo takribani vijana 5000 kutoka nchi 52 za Afrika walishindanishwa katika vipengele mbalimbali.
Tuzo hizo zinawatambua vijana wajasiriamali bora, wanaharakati, waleta mabadiliko na wafuatiliaji ambao wameonyesha ubora wa kipekee katika nyanja zao.
Video Nzima ipo katika Akaunti yetu ya Youtube ya Bongo5
Written and edited by #abbrah255 and @yasiningitu