Kauli ya Rais wa Uganda Museveni kuhusu mlipuko wa jana

 

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne usiku saa kadhaa baaada ya mashambulio hiyo ambapo alitumia majini ya wanyama kuwakemea na kutaja majina yao.

“Mlipuaji wa CPS alifahamika kama Mansur Othman na yule aliyejilipuakatika ofisi za IGG anaitwa Wanjusi Abdalla,” rais alisema.

Aliongeza kuwa maelezo yalipatikana kutoka mtu wa tatu ambaye pia alikuwa mlipuaji wa kujitoa mhanga ambaye walinzi walimkamata Bwaise lakini alibainisha kuwa baadaye alikufa kutokana na majeraha ya risasi aliyopata wakati wa kukamatwa kwake mapema Jumanne.

Rais aliwataja washambuliaji hao wa kujitoa mhanga waliokufa kama waathiriwa wa machafuko, kuwalaumu walioshawishi kuwa na msimamo mkali na kuwataja nguruwe.

“Nguruwe halisi ni watu kama Nsubuga, yule anayeitwa Sheikh aliyewachanganya vijana kule Lweza. Iwapo kujilipua kutampeleka peponi, ajilipue kama mfano badala ya kuwadanganya watoto wadogo,” Museveni alisema.

Related Articles

Back to top button