HabariMichezo

Kazi kwenu wachezaji wa Yanga

Klabu ya Yanga SC inatarajia kushuka dimbani Leo nchini Rwanda,Kigali kuwavaa Al Merreikh ya Sudan ambao wamechagua Rwanda kama nyumbani kwao,kuelekea mchezo huu deni pekee limebaki kwa wachezaji wa Yanga kuhakikisha Wanafikia malengo kwa kufanya vizuri kwanza kuendelea walipoishia msimu uliopita katika mashindano ya kimataifa kwa kufanya vizuri kombe la Shirikisho kwa kucheza fainali .

Jambo la pili mashabiki na wanachama wa Yanga wamefanya kazi Yao Tena katika kiwango kikubwa wameenda wengi sana nchini Rwanda kuanikiza ushindi bila kujali chochote wamesafir umbali mrefu huo ni upendo mkubwa ambao wachezaji wanatakiwa kuwalipa kwa matokeo mazuri uwanjani Leo.

Pia kwa mujibu wa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema swala la bonus ni kama kawaida Siku zote mzigo upo kama walivyo kubaliana hiyo maanake viongozi wamefanya Kila kitu kuhakikisha mambo yanaenda sawa kwahiyo jambo muhimu wachezaji wanatakiwa kupambana kwa jasho na damu kahakikisha wanapata matokeo mazuri hili kuwafuraisha mashabiki zao wengi waliosafiri kuwaunga mkono.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents