Michezo

Kelvin John ‘Mbappe’: ”Naitaka Ballon d’Or, Genk wananihitaji tatizo Umri, nataka kuwa zaidi ya Mbappe ”(+video)

Nyota wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Kelvin Pius John kwa jina la utani ‘Mbappe’ amefunguka juu ya maisha yake ya soka huku kubwa akieleza namna alivyopambana mpaka kufikia hapo alipo fika leo hii.

Akizungumza na TFF TV, Kelvin John amesema kuwa baba yake mzazi hakuwa akipenda kumuona akicheza mpira na badala yake alihitaji asome.

”Baba yangu alikuwa anapinga sana kitendo cha kuniona nacheza mpira yeye alitana nisome hasa kutokana nilikuwa na umri mdogo, lakini mimi nilikuwa simuelewi, hata akinipiga mimi naenda tena mazoezini. Baadae mwalimu mkuu akaongea na baba ndio akaniruhusu tena kishingo upande.”

Kelvin John ‘Mbappe’ amezungumzia dili lake na klabu ya KRC Genk ya Mbwana Samatta pamoja na ndoto zake katika mchezo huo wa soka.

”KRG Genk wananihitaji, walikuwa wananifatilia kabla ya AFCON na hata baada lakini kilichokuwa kinashindikana ni kwasababu umri wangu bado mdogo ikabidi watulie kwanza.”

”Wameongea na meneja wangu, ikabidi nisafiri kuelekea Ubelgiji nikaenda kule wakasema wananihitaji, lakini kwa sasa hivi inakuwa ngumu kunichukua kutokana sijafikia umri wa kusaini kwahiyo wakabidi wasubiri mpaka nitakapofikisha umri wa miaka 18. Tanzania zipo timu zinazonihitaji lakini malengo yangu ni kucheza Ulaya.”

”Kinacho nisumbua katika akili yangu ni kuja kuchukua tuzo ya Ballon d’Or ninaimani itatimia nia ninayo, uwezo ninao na kila kitu ninacho. Nawashukuru Watanzania kwa heshima kubwa waliyonipa kwa kunipatia jina la Kylian Mbappe sijafikia katika mafanikio yake lakini nataka niwe zaidi yake”.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents