Kenya haitakubali kutoa hata inchi moja ya ardhi yake kwa Somalia – Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya kuwa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa wa kuipatia Somalia eneo kubwa la bahari linalogombaniwa kutoka pwani ya nchi yao itafanya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kudorora.

Kenyatta alipinga uamuzi huo wa eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi akisema watageuza faida za kisiasa na kiuchumi, na kutishia usalama katika Pembe dhaifu la Afrika.

Amesisitiza wito wake wa kuwepo kwa suluhu ya mazungumzo katika mzozo huo.

Awali rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohammed maarufu farmajo aliitaka Kenya kuheshimu sheria ya kimataifa baada ya mahakama hiyo ya Umoja wa Kimataifa kukabidhi umiliki wa eneo kubwa linalodaiwa kuwa na mafuta na gesi katika bahari hindi kwa Somali.

Katika hotuba iliokwenda moja kwa moja katika runinga baada ya uamuzi huo, Mohamed Abdullahi Mohamed, alisema kwamba Nairobi inapaswa kuona uamuzi huo kama fursaya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Mnamo 2009, nchi hizo mbili zilikubaliana katika hati ya makubaliano, ikiungwa mkono na UN, kumaliza mzozo wa mipaka kupitia mazungumzo.

Lakini miaka mitano baadaye, Somalia ilisema mazungumzo yalishindwa na badala yake ikaenda kwa ICJ.

Mwaka 2014, Somalia iliamua kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo katika mahakama ya kimataifa ya (International Court of Justice) iliyoko Hague.

Katika ombi lake, Somalia ilisema mazungumzo ya kidiplomasia yameshindikana na sasa mahakama “iamue uratibu sahihi wa kijiografia wa mpaka mmoja wa baharini katika Bahari ya Hindi”.

Lakini hayo si yote. Somalia iliitaka mahakama ya kimataifa ICJ kutangaza kuwa “Kenya… imekiuka wajibu kimataifa wa kuheshimu haki za nchi na mahakama”.

Mwaka mmoja baadae , Kenya iliweka upingamizi mahakamani juu ya kesi hiyo.

Related Articles

Back to top button