Kenya ilivyopokea shehena yenye chanjo ya Corona ya kwanza na kuungana na mataifa haya Afrika (+ Video)

Nchi nyingi zaidi Afrika zimepokea chanjo ya kwanza ya virusi vya corona chini ya mpango wa Covax duniani Kenya imepokea dozi milioni 1.02 za chanjo ya Oxford-AstraZeneca Jumatano, na kuwa nchi ya tatu ta Afrika Mashariki kunufaika na mpango huo.

Ndege iliyobeba chanjo ikiwasili nchini Kenya
Image caption: Ndege iliyobeba chanjo ikiwasili nchini Kenya

Dozi zilizopatikana zinatosheleza watu 500,000 katika awamu ya kwanza.

Wafanyakazi wa afya waliomstari wa mbele kattika tiba ya corona, walimu, maafisa wa polisi na watu wazima watakuwa kundi la kwanza kupata chanjo hiyo.

Katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Waziri wa afya Eteni Longondo alikuwa uwanja wa ndege Jumanne usiku kupokea dozi milioni 1.7 za chanjo ya AstraZeneca.

Waziri akipokea shehena ya chanjo DRC
Image caption: Waziri akipokea shehena ya chanjo DRC

DR Congo inatarajia jumla ya dozi milioni 6.9 kuwasilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa Mei 2021.

Shehena ya chanjo ikipokelewa DRC
Image caption: Shehena ya chanjo ikipokelewa DRC

Angola imepokea dozi 624,000 za chanjo huku Gambia ikiwa imepokea dozi 36,000 Jumatano.

Mpango wa Covax wa Shirila la Afya Duniani (WHO) ulilenga utoaji wa chanjo ya virusi vya corona kwa usawa kote duniani.

Ina matumaini ya kuwasilisha zaidi ya dozi bilioni mbili kwa watu katika nchi 190 chini ya mwaka mmoja.

Nchi za Afrika zaendelea kupokea chanjo ya corona

Wakati huo huo, Jumatano asubuhi, Rwanda imepokea dozi yake ya kwanza ya chanjo ya Oxford-AstraZeneca huku ikitarajia dozi 102,960 za chanjo ya Pfizer, kulingana na wizara ya afya.

Chanjo zote mbili zitatumika kwa jumla ya watu 171,480 waliotambuliwa kama kundi lililo katika hatari zaidi ambalo litapewa kipaumbele huku utoaji wa chanjo hiyo ukianza Ijumaa, wizara imesema katika taarifa.

Rwanda inatarajia kupokea jumla ya chanjo 1,098,960 za AstraZeneca na Pfizer, katika mpango wa Covax unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

“Lengo letu ni kutoa chanjo hiyo kwa asilimia 30 ya watu kufikia mwisho wa mwaka 2021, na asilimia 60 ya watu kufikia mwisho wa mwaka 2022”, Waziri wa afya wa Rwanda Dkt. Daniel Ngamije amesema.

Rwanda imeripoti zaidi ya maambukizi 19,000 ya virusi vya corona huku idadi ya waliofariki dunia ikiwa ni 265.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CL9AM8RBqFD/

Related Articles

Back to top button