Afya

Kenya kupokea chanjo ya corona wiki lijalo

Kenya itapokea bachi ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 wiki ijayo, baraza la mawaziri limesema. Wahudumu wa afya, maafisa usalama, waalimu na watu walio kwenye hatari watakuwa wa kwanza kupatiwa chanjo hiyo.

Serikali haijaeleza kwa kina ni chanjo gani wanayoitarajia.

Kwa mujibu wa BBC. Wizara ya Afya awali mwezi huu ilisema ilifuatilia chanjo ya AstraZeneca na kuidhinisha kwa matumizi nchini humo.

Kenya mpaka sasa imerekodi wagonjwa 105,057 wa virusi vya corona, kwa mujibu wa data za Wizara ya Afya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents