Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMahojiano

Kesi ya Mwijaku na Nandy yanguruma mahakama ya Mwanzo, Hakimu adai haya

Kesi inayomkabili msanii wa Bongo Fleva Faustina Charles Mfinanga alimaarufu Nandy imeendelea katika mahakam ya mwanzo Sinza jijini Dar Es Salaam siku ya leo tarehe 12-8-2022.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa na Mtangazaji wa Clouds FM Burton Mwambe alimaarufu kama Mwijaku kwa madai kuwa alitumiwa vibaya na Nandy pasina makubaliano yake.

Mwijaku ameieleza mahakama kuwa, walielewana na Nandy afanye Tangazo kwa ajili ya Nandy Festival ambapo Tangazo hilo lilifanyika Hospitalini na baada ya Tangazo kukamilika Nandy alilikataa Tangazo hilo ila baada ya muda alikuta Nandy amelipost na wakashindwa kuelewa hivyo akaaumua kwenda mahakamani.

Kesi hiyo ilisikilizwa tarehe 9-8-2022 na ilipigwa tarehe mpaka leo tarehe 12-8-2022, baada ya Mwijaku kufika na Wakili wake pia Nandy kuwakilishwa na Meneja wake pamoja na wakili imepigwa tarehe tena mpaka tarehe 19-8-2022 hapo hapo mahakama ya Mwanzo.

Hakimu ameomba wahusika yaani mshitaki na mshitakiwa waje na nyaraka stahiki ikiwemo mkataba waliosaini kwa ajili ya Tangazo hilo, endapo mmojawao ataonekana ameenda kinyume na mkataba ule basi atamlipa mwenzake na madai ya Mwijaku ni kwamba anamdai Nandy milioni 10.

Related Articles

Back to top button