Habari

Kesi ya Zuma kuendelea leo licha ya vurugu Afrika Kusini

Kesi ya muda mrefu ya rushwa inayomkabili rais wa zamani wa Afrika Kusini aliyeko jela Jacob Zuma itaendelea leo kwa njia ya video, licha ya vurugu kali ambazo zimelikumba taifa hilo baada ya kufungwa jela katika kesi nyingine.

Zuma anakabiliwa na mashitaka 16 ya ulaghai na rushwa kuhusiana na manunuzi ya  mwaka wa 1999 ya  ndege za kivita, boti za kushika doria, na vifaa vya Jeshi kutoka kwa kampuni tano za kijeshi barani Ulaya wakati akiwa Naibu Rais wa Afrika ya kusini.

Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kupokea hongo kutoka kwa moja ya kampuni za kigeni, Thales ya Ufaransa, ambayo ilishitakiwa kwa rushwa na utakatishaji pesa. Kesi hiyo ilianza Mei baada ya kuahirishwa na kucheleweshwa mara kadhaa, wakati timu ya utetezi ya Zuma ikipambana kutaka mashitaka hayo yafutwe. Zuma mwenye umri wa miaka 79, anasisitiza hana hatia. Kampuni ya Thales pia ilikana mashitaka.

Jacob Zuma kwa sasa yupo katika moja ya magereza nchini Afrika Kusini, akitumikia kifungo chake cha miezi 15 alichohukumiwa hivi karibuni.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents