HabariMichezo

Kibu, Inonga faini laki tano kila mmoja

Baada ya kufunga bao pekee la klabu ya Simba katika mchezo huo, mchezaji, Kibu Denis alitenda kosa la kwenda kushangilia mbele ya jukwaa la mashabiki wa Yanga kwa kuonesha ishara ya kuwafunga mdomo.

Kamati imemtoza faini ya Sh. 500,000 (laki tano) mchezaji Kibu Denis kwa mujibu wa Kanuni ya 17:(14 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Kamati imemtoza faini ya Sh. 500,000 (laki tano) mchezaji Henock Inonga wa klabu ya Simba kwa kosa la kwenda kushangilia bao mbele ya maafisa wa benchi la ufundi la klabu ya Yanga.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:(14 & 60) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents