Habari

Kiingereza cha Msukuma Bungeni wabunge washindwa kujizuia (+Video)

Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma akiuliza swali kwa Kiingereza kwa mgombea Ubunge wa Afrika Mashariki Mhandisi Mohamed Mnyaa wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Baada ya Spika Tulia Ackson kumtaja Musukuma kuuliza swali kwa mgombea huyo, wabunge wameibua shangwe na kugonga meza huku baadhi wakimtuza fedha kutokana na umahiri wake wa kuulizwa swali kwa lugha ya kiingereza.

Mbunge Musukuma amemuuliza Mnyaa kuwa “kwa kipindi cha miaka mitano amefanya nini mpaka aombe tena kuchaguliwa katika Bunge hilo?.”

Hata Spika wa Bunge Dk Tulia Akson aliweka mambo sawa kwa kulirudia swali alilouliza Msukuma ili Mhandisi Mohamed Mnyaa aweze kuelewa.

Mara kadhaa Mbunge Musukuma amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akisema elimu yake ni darasa la saba, lakini ana uwezo mkubwa kulinganisha na wale wanaojiita wasomi.

Related Articles

Back to top button