Habari
Kijana mwenye ulemavu akimbiza kidato cha sita, ashika nafasi ya 3 kati ya Wanafunzi 28 (Video)
“Ulemavu sio kushindwa, bali kushindwa ni ulemavu”.
Kauli hiyo imethibitoshwa na Kijana mwenye ulemavu wa viungo Erick Nyanda ambaye amefanya vizuri katika masomo ya kidato cha sita biashara namkufanya ashike nafasi ya 3 kati ya wanafunzi 28 kwa akupata division 1 ya point 5.
Nyanda (20) licha ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kuzaliwa nao Congenital Scoliosis ‘Kibiongo’ ambao huathiri uti wa mgongo, kwake haikuwa kikwazo katika kutimiza malengo yake.