Habari

Kikapu kilichojaa matunda kwa zaidi ya miaka 2000 chagunduliwa chini ya bahari

Kikapu kilichojaa matunda ambacho kimekuwepo kwa miaka zaidi ya 2,000 kimegundulika chini ya bahari miongoni mwa mabaki ya zamani katika mji wa kale wa Thonis-Heracleion, pwani ya Misri.

Mamia ya vitu vya kufinyangwa na shaba ni kati ya vitu vingine ambavyo vimegunduliwa karibu na mji wa Alexandria.

Eneo la kale la Thonis-Heracleion lilitoweka chini ya maji baada ya mfululizo wa majanga ya asili. Mji huo uligunduliwa miongo miwili iliyopita.

Tangu wakati huo umekuwa ukitoa utajiri mwingi wa hazina zikiwemo sanamu kubwa. Inakadiriwa kuwa 3% pekee ya eneo hilo limefanyiwa utafiti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents