HabariSiasa

Kikongwe aliyecheza na Obama afariki dunia

Mwanamke wa Washington DC ambaye aliifanikisha ndoto yake ya kucheza densi na Rais Barack Obama katika Ikulu ya White House amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 113.

Virginia McLaurin alikuwa na umri wa miaka 106 alipokutana na rais wa kwanza mweusi na mke wake mwaka wa 2016.

“Wacha nikwambie, Nina furaha sana,” alimwambia Rais Obama wakati huo. “Rais mweusi, yay, na mke wake mweusi.”

Mwaka 2014, ajuza huyo alianzisha ombi la mtandaoni kutaka kumuona. “Jina langu ni Virginia McLaurin,” aliandika, “Naishi Washington DC. Nilizaliwa mwaka 1909.”

“Sijawahi kukutana na Rais. Sikuwahi kufikiria ningemuona Rais mweusi wa nilizaliwa Kusini na sikufikiri ingetokea. “Nina furaha sana na ningependa kukutana nawe na familia yako ikiwezekana.”

Mshonaji huyo wa zamani aliendelea: “Nakumbuka nyakati za kabla ya Rais Hoover. “Nakumbuka hatukuwa na umeme, niltumia taa ya mafuta ya taa, nakumbuka gari la kwanza la Ford.

“Mume wangu alikuwa katika Jeshi. Nilimpoteza mume wangu mwaka wa 1941. Nimekuwa DC tangu wakati huo. Nilikuwa nikiishi hapa wakati Martin Luther King aliuawa.”

Related Articles

Back to top button