Burudani

Kikwete ashukuru Marioo kumpa mtoko (Video)

“Maisha yetu yamekuwa magumu kidogo”

 

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye usiku wa @marioo_tz ambapo alionyesha kushukuru kupewa mualiko kwani ndio fursa pekee aliyokuwa nayo yakutoka usiku.

“Mnanipatia mitoko maana maisha yetu wengine yamekuwa magumu kidogo,” Alisema Kikwete.

Aliongeza,”Unaishi nyumba inaukuta mkubwaaa wa nje, kuna ukuta wa katikati halafu kuna ukuta wa nyumba unayoishi wewe, na hawa jamaa ndio kama unavyowaona, kila ulipo wapo. Kwahiyo unavyopata Maulidi kama huu ndio unapata nafasi yakutoka usiku,”

Kikwete amesema anapenda burudani ya muziki ndio maana akipewa mialiko anafurahi.

Show ya mwisho kuhudhuria ilikuwa ni ya uzinduzi wa albamu ya Ommy Dimpoz, Disemba Mwaka 2022, Johari Rotana Dar Es Salaam.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents