Michezo

Kili awards 2012 Nominees hawa hapa!

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo wametangaza rasmi wateule wa vinyang’anyiro 22 vya Tunzo za Muziki Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Awards) kwa mwaka 2012.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=j3XiAeceXCo[/youtube]

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bwana George Kavishe alisema “Academy ilikaa mwisho wa wiki iliopita na kufanya kazi ngumu na nzuri ya kuteua wasanii wa muziki waliofanya kazi nzuri na zilizopendwa na kukubalika zaidi na wengi kwa mwaka 2011”.

Mchakato wa Academy ulisimamiwa na wasimamizi wa mahesabu na utawala INNOVEX ili kuhakikisha zoezi linafanywa kwa uhuru na haki muda wote. George Kavishe aliongeza “Kama tulivoahidi mwaka juzi na mwaka jana kwamba tuzo zitaendeshwa kisasa na kitaalum ili kuzipatia haki na kutengeneza mazingira ya uwazi kwa wapenzi wa muziki nchini. Tunaendeleza ahadi hii na ndio maana INNOVEX wameendelea kusimamia zoezi hili la Academy pamoja na kura zote kwa mwaka huu tena.”

Kura za wana Academy ni siri na majibu ya wateule watano kwa kila kinyang’anyiro hubaki siri ya INNOVEX hadi kutangazwa, halikadhalika na majibu ya kura za wananchi za washindi.

Baraza la Sanaa Tanzania kupitia kwa mwakilishi wake Nd. Angelo Luhala ambaye ni mratibu wa Tuzo za Muziki Tanzania, nalo limeipongeza Academy kwa kazi nzuri kwa mara ingine na kuwasii wasanii kuyapokea matokeo na kushirikiana na waandaji katika hatua zilizobakia ili kufanikisha tuzo hizi.
Hatua zifwatazo:

1. Semina ya Wasanii:
Wasanii wateule wa tuzo mbalimbali watapata semina elekezi kuhusu tuzo hizi na kupata nafasi kuuliza maswali juu ya mchakato mzima wa kupata wateule na taratibu zitakazofwata.
2. Kura.
Kura zitapigwa kwa muda wa wiki 7 kuanzia tarehe 13/ Feb – 06/ Apr Maelekezo ya upigaji kura yatapatikana katika tovuti ya Kilimanjaro www.kilitimetz.com na mitandao mingine pamoja na kwenye matangazo ya magazeti na vipindi mbali mbali ya redio na TV.
3. Usiku wa utoaji Tuzo.
Kilimanjaro Tanzania Music Awards zatarajia kufanyika tarehe 14. Aprili. 2012 katika ukumbi wa Mlimani City. Taarifa zaidi zitafuata kupitia mitandao, redio na TV mbali mbali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents