Habari

Kilimanjaro: Mwanamke auawa na tembo

Saumu Hassan mwenye umri wa miaka 32, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na tembo akiwa shambani katika kitongoji cha kijiweni wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema tukio hilo lilitokea farehe 19 mwezi huu majira ya asubuhi wakati mwanamke huyo akiwa shambani akichimba viazi.

Amesema mwanamke huyo alikutwa amefariki dunia baada ya kujeruhiwa na tembo, ambapo alipata majeraha makubwa kwenye mwili wake.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Maigwa ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari pindi wanapokwenda shambani, hasa wale ambao wamepakana na hifadhi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents