Habari

Kim Jong Un kuimarisha uhusiano na China

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema leo kuwa analenga kuimarisha zaidi mahusiano yake na China wakati anajaribu kuikwamua nchi yake kutoka mzozo mkubwa unaohusishwa na janga la virusi vya corona.

Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeripoti kuwa Kim ametoa matamshi hayo kupitia ujumbe wa pongezi alioutuma kwa rais Xi Jinping wa China kwa maandimisho ya miaka 100 tangu kuundwa kwa chama cha kikomunisti cha China.

Kim amenukuliwa akisema chama tawala cha kikomunisti cha Korea Kaskazini kwa kushirikiana na chama tawala cha China kitaimarisha urafiki kati ya Pyong-Yang na Beijing katika kiwango cha juu kwa kuzingatia zama za sasa na mahitaji ya raia wa pande mbili.

China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini na ni miongoni mwa mataifa machache ambayo hayatekelezi kikamilifu vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya Pyong-Yang kutokana na mradi tata wa silaha za nyuklia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents