Habari

Kimbunga Fiona chapiga Puerto Rico

Kimbunga Fiona kimepiga eneo la Kusini Magharibi la Puerto Rico jana Jumapili huku kikisababisha maporomko ya tope, kuharibu gridi ya taifa ya umeme na kung’oa mapande makubwa ya lami barabarani na kuyatawanya katika maeneo mbalimbali.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema kimbunga hicho huenda kikasababisha mafuriko makubwa na kitisho cha viwango vya kihistoria vya mvua kubwa hadi kufikia sentimita 64 katika baadhi ya maeneo.

Gavana wa Puerto Rico Pedro Pierluisi amesema uharibifu ulioshuhudiwa umefikia kiwango cha janga.

Kimbunga Fiona kimelisomba daraja moja katika mji wa kati wa milima wa Utuadi ambalo polisi wanasema lilijengwa na jeshi la taifa kufuatia kimbunga Maria mnamo 2017.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents