Habari

Kimbunga Ida chapiga Louisiana

Kimbunga Ida, kilichoainishwa na wataalam wa hali ya hewa kama ni “hatari sana”, kimepiga katika jimbo la Louisiana nchini Marekani.

Kimbunga hicho kinavuma na upepo wa hadi kilomita 240 kwa saa moja katika mji wa New Orleans kulingana na Kituo cha Kimbunga cha Kitaifa.

Wakazi wengi wa jimbo hilo walioshikwa na hofu wanajaribu kukimbia. Na Serikali imewataka watu wanaoishi kwenye maeneo ya pwani waondoke na kwenda kwenye maeneo salama.

Ni miaka 16 tangu siku kilipotokea Kimbunga “Katrina” mjini New Orleans.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents