Kinachoendelea katika tetesi za usajili Ulaya

Manchester United wameambiwa kuwa itawagharimu kiasi cha pauni milioni 81.5 kumsajili winga Jadon Sancho,21, kutoka Borussia Dortmund. (Mirror)

Talks continue between Man Utd and Borussia Dortmund over the signing of Jadon Sancho

Tottenham itafanya mazungumzo zaidi na kocha wa Ajax Erik Ten Hag,51, baada ya kushindwa kufanikisha uhamisho wa Antonio Conte. (Mirror)

Tottenham itafanya mazungumzo zaidi na kocha wa Ajax Erik Ten Hag

Duncan Ferguson, 49, amekataa kazi ya ukufunzi Real Madrid kwasababu atanaka kuwa kocha wa Everton. (Sun)Duncan Ferguson, 49, amekataa kazi ya ukufunzi Real Madrid

West Ham wanaamini kuwa David Moyes atasaini mkataba mpya wa kudumu baada ya kufanya mazungumzo na kocha huyo ambaye amehusishwa na tetesi za kurejea Everton. (Football Insider)

West Ham wanaamini kuwa David Moyes atasaini mkataba mpya wa kudumu

Mlinzi wa kulia wa Atletico Madrid Kieran Trippier,30, amewaambia wachezaji wenzake wa England yuko na mpango wa kujiunga na Manchester United msimu huu. (Mirror)

Barcelona wanafikiria kutoa ofa iliyoboreshwa kwa kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum,30, ambaye anajiandaa kuondoka Liverpool kwa uhamisho huru, baada ya Paris St-Germain kupoteza ofa ya awali ya Barca.(Marca – in Spanish)

Ikiwa Barcelona haitakamilisha usajili wa Wijnaldum na Memphis Depay, 27, wa Uholanzi kutoka Lyon wiki ijayo inaweza kuwauza hadi wachezaji wanne. (Sport – in Spanish)

Mlinzi wa kulia wa Atletico Madrid Kieran Trippier,30, amewaambia wachezaji wenzake wa England yuko na mpango wa kujiunga na Manchester United

Juma lijalo Barca itaongeza mkataba wa muda mrefu wa Ilaix Moriba, kiungo wa kati wa Uhispania mwenye miaka 18 aliyebaki na mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa na amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Manchester City au Manchester United. (Marca-in Spanish)Georginio Wijnaldum anajiandaa kuondoka Liverpool kwa uhamisho huru

Kocha mpya wa Roma Jose Mourinho anataka kumsajili mmoja kati ya walinda mlango watatu: Hugo Loloris,34, wa Tottenham, Wojciech Szczesny, 31, wa Juventus au Rui Patricio wa Wolves,33. (La Gazetta dello Sport-in Italian)

Mchezaji wa Arsenal Granit Xhaka, 28, anasalia kuwa mtu anayelengwa zaidi na Roma katika eneo la kiungo wa kati. (Corriere dello Sport-in Italian)Leeds United imepewa nafasi ya kumsajili Eddie Nketiah msimu huu, Arsenal ikitaka kitita cha pauni milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji hyo mwenye miaka 22. (Football Insider)

Atletico Madrid wanatarajiwa kutoa ofa mpya kwa kiungo wa kati Rodrigo de Paul,27, ambaye pia amekuwa akihusishwa na timu za Liverpool na AC Milan. (Mundo Deportivo- in Italian)

Leicester wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Boubakary Soumare

Leicester wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Boubakary Soumare,22, anayekipiga Lille na wameendelea kuvutiwa na Tammy Abraham ikiwa mshambuliaji huyo wa England, 23, ataondoka Chelsea msimu huu. (Leicester Mercury)

Leeds United na Brighton wamejiunga na Rangers katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Sparta Rotterdam Abdou Harroui,23, (Football Insider)Burnley na Norwich ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Primia ambavyo vimeiomba Liverpool kuhusu kumnyakua beki wa kulia wa Wales Neco Williams,20, kwa mkopo msimu ujao. (Teamtalk)

West Brom wamemwambia kiungo wa kati wa Brazil Matheus Pereira,25, kuwa anaweza kuondoka msimu huu isipokuwa kwa masharti

Brentford ina mpango wa kumsajili mlinzi wa kushoto Gabriel Fuentes,24, kutoka Junior FC . (Sun)West Brom wamemwambia kiungo wa kati wa Brazil Matheus Pereira,25, kuwa anaweza kuondoka msimu huu iwapo watapewa kiasi cha angalau pauni milioni 15. Aston villa na Brighton ni miongoni mwa timu zinazomfuatilia mchezaji huyo. (Teamtalk)

Kocha wa Lincoln City Michael Appleton, mwenye umri wa miaka 45, ndiye kipaumbele kuchukua nafasi West Brom, baada ya Waggies kusitisha mipango ya kumteua Chris Wilder. (Football Insider)

Kocha wa Bournemouth Jonathan Woodgate, 41, yuko hatarini kutimuliwa, huku kocha wa Fulham Scott Parker 40, akiwa kwenye orodha ya wanaotakiwa kuchukua nafasi yake. (Sun)

Related Articles

Back to top button