HabariSiasa

Kinana akerwa na Trafiki kusimamisha magari kila saa, ampa ushauri IGP Wambura (+Video)

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Komredi Abdulrahman Kinana amemshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camilius Wambura, kufanya tathimini ili kuona kama inawezekana kupunguza idadi ya askari wa usalama barabarani ambao wamekuwa wakilalamikiwa kusababisha kero kwa wananchi.

Kinana ametoa ushauri huo Julai 27,2022 akiwa katika mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ya mikoa ya Songwe na Mbeya dhidi ya idadi kubwa ya askari wa barabarani ambao wamekuwa wakiwasimamisha mara kwa mara, hivyo kucheleshewesha shughuli za maendeleo.

Malalamiko hayo ya wananchi yaliendelea kuibuka hata kwenye kikao cha ndani cha Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe ambapo mmoja wa wanachama wa Chama hicho ambaye ni dereva wa magari ya kubeba abiria maarufu kama Costa, kutoa malalamiko yake mbele ya Kinana akidai wamechoka kusimamishwa mara kwa mara na matrafiki na kila wanaposimama wanatozwa Sh. 2000 kwa kila kituo.

Related Articles

Back to top button