Habari

Kiongozi maarufu wa upinzani Urusi Alexei Navalny akumbwa na ugonjwa huu wa ajabu,asema ” nilihisi nimepewa sumu”

Kiongozi maarufu wa upinzani Urusi Alexei Navalny akumbwa na ugonjwa wa ajabu,yeye asema " nilihisi nimepewa sumu"

Kiongozi maarufu wa upinzani Urusi, Alexei Navalny, ametoka hospitalini alikokuwa amelazwa Moscow baada ya ripoti za awali kuashiria kuwa alikabiliwa na mzio mkali .

Kwa mujibu wa BBC. Ulimfanya uso kufura, kutokwa na maji machoni na vipele mwilini. Daktari wake binafsi siku ya Jumapili amesema, Navalny hajawahi kukabiliwa na mzio katika siku za nyuma na huenda amekumbana na ‘kitu chenye sumu’.

Katika taarifa aliyoiandika Kirusi kwenye blogu yake na aliyoiandika kutoka gerezani, Navalny amesema hajawahi kukabiliwa na mzio maishani mwake. Ameongeza kwamba mkewe hupata tatizo hilo kwahiyo anafahamu namna linvyokaa.

“Usiku niliamka nikihisi joto jingi na kudungwa usoni, masikioni na shingoni,” aliandika. “Nilihisi kama ambaye uso wangu umesuguliwa kwa pamba ya glasi.”

“Fikra ilinijia, pengine nimepewa sumu.”

Navalny alifungwa gerezani kwa siku 30 wiki iliyopita kwa kuandaama maandamano kinyume cha sheria kupinga kutengwa kwa wapinzani kutoka uchaguzi wa kieneo ambapo takriban watu 1,400 walizuiwa.

Mwanaharakati huyo mwenye miaka 43 aliwahi kufungwa mara kadhaa katika siku za nyuma, lakini tunafahamu nini kuhusu mpinzani huyo maarufu Urusi mkosoaji wa rais Vladimir Putin?

” Wahalifu na wezi

Amekitaja chama cha Putin kama sehemu ya “wahalifu na wezi”, na kuushutumu mfumo wa rais kwa ‘kuinyonya Urusi damu’ na kuahidi kuangamiza alichokitaja kuwa ni kuidhinishwa kwa ‘taifa la wenye nacho’.

Ameongoza maandamano ya kitaifa kupinga utawala.

Kremlin critic Alexei Navalny, who was arrested during March 26 anti-corruption rally, gestures during an appeal hearing at a court in Moscow on March 30, 2017.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNavalny wakati wa kusikizwa rufaa Moscow mnamo Machi 2017, baada ya kukamatwa katika kampeni ya kupinga ufisadi

Lakini hajafanikiwa kutimiza ambacho pengine ndio ndoto yake kubwa: kumpinga Putin katika debe la uchaguzi.

Alipigwa marufuku kugombea katika uchaguzi mnamo 2018 kwa kushtakiwa kwa ufujaji wa fedha , kesi inayomzuia kuwania wadhifa serikalini.

Navalny anakana vikali thuma hizo akisema matatizo yake kisheria ni njia ya Kremlin kumuadhibu kwa ukosoaji wake mkali.

Kuibuka kwake kama nguvu katika siasa za Urusi kulianza mnamo 2008 alipoanza kuandika katika blogu kuhusu makosa ya utendaji na ufisadi katika baadhi ya mashirika makubwa nchini.

Ametumia mitandao ya kijamii kuwasilisha mbinu yake ya kisiasa, kuwavutia vijana kwa lugha kali, na kukebehi taasisi zinazomtii Putin, anayekataa kulitaja jina lake.

Upinzani wa moja kwa moja

Kampeni dhidi ya ufisadi ilimpeleka Navalny kutoka kuwa mkosoaji wa mashirika na kuwa mpinzani wa moja kwa moja kwa chama tawala.

Kufuatia kuwadia uchaguzi wa ubunge wa 2011, aliwaomba wasomaji blogu yake kukichagua chama kingine chochote ila sio chama tawala United Russia, alichokitaja kuwa “chama cha wahalifu na wezi”. Kauli iliyopata umaarufu.

United Russia kilishinda uchaguzi huo, lakini kwa uwingi mdogo na ushindi huo uligubikwa kwa tuhuma za udanganyifu uliochangia kuzuka maandamano mjini Moscow na katika miji mingine mikubwa.


Alexei Navalny: Ni nani?

Police officers detain Russia's top opposition figure Alexei Navalny (C) after his visit the city's election commission office to submit documents to get registered as a mayoral election candidate in Moscow July 10, 2013.

Navalny alikamatwa na kuwekwa gerezani kwa siku 15 kufuatia maandamanoya kwanza mnamo Desemba 5 2011 lakini akabuka kuzungumza katika mkutano mkubwa wa kisiasa baada ya uchaguzi Moscow Desemba, uliohudhuriwa na watu 120,000.

Putin alichaguliwa tena kama rais kwa urahisi na kamati yenye nguvu ya uchunguzi nchini ikaidhinisha uchunguzi dhidi ya shughuli za Navalny za siku za nyuma, kiasi cha hata kuhoji sifa yake ya uwakili.

Alipokamatwa kwa muda mfupi mnamo Julai 2013 kwa ubadhirifu wa fedha katika mji wa Kirov, hukumu hiyo ya miaka mitano ilitazamwa pakubwa kama ya kisiasa.

Aliachuliwa huru ghafla kupiga kampeni kwa uchaguzi wa u Meya Moscow, iambapo alipata 27% ya kura nyuma ya mshirika wa Putin, Sergei Sobyanin.

Huo ulitazamwa kama ufanisi kutokana na kuwa ushindi wake ulitokana na intaneti na kwa kuzungumza na watu pekee.

Alexei Navalny returns from Kirov after his 5-year term was made a suspended sentenceHaki miliki ya pichaAFP

Kesi yake ikageuzwa na mahakama ya juu zaidi Urusi kufuatia uamuzi wa mahakama ya haki za binaadamu ya Ulaya kwamba kesi yake haikusikizwa kwa usawa.

Alafu katika kusikizwa tena 2017, alishtakiwa kwa mara ya pili na kupewa hukumu ya baadaye ya miaka mitano.

Alitaja hukumu hyo kama jitihada ya kumzuia kuwania katika uchaguzi mkuu wa 2018.

Police officers detain protest leader Alexei Navalny outside Zamoskvoretsky district court in Moscow, on 24 February 2014Haki miliki ya pichaAFP
Image captionNavalny amekamatwa mara kadhaa katika miaka ya nyuma

Afya yake sasa

Madaktari wanamfanyia ukaguzi hivi sasa kubaini chanzo cha kuugua kwake ghafla baada ya kukamatwa hivi karibuni.

Ripoti za awali zinaashiria alipata mzio mkali zilizochangia uso wake kufura macho kutoka maji na kutokwa na vipele mwilini.

Hatahivyo, daktari binafsi wa Navalny siku ya Jumapili amesema hajawahi kukabiliwa na mzio katika siku za nyuma na huenda amekumbana na ‘kitu chenye sumu’.

Maafisa wa afya waliomhudumia wanasema walifanikiwa kumtibu Jumatatu, na wamepanga ukaguzi wa kando wa sampuli za nywele zake na fulana aliovaa .

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents