Habari

Kiongozi mpya Kanisa Katoliki duniani ni Papa Leo XIV

Kardinali Robert Francis Prevost OSA ametangazwa kuwa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani na amechagua jina la Papa Leo wa XIV (14).

Papa Leo wa XIV ametangazwa leo na Kardinali Dominique Mamberi mara baada ya makardinali wapatao 133 kumaliza kupiga kura ya kumchagua.

Shangwe na nderemo zimetawala katika uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Petro Vatican wakati watu wakishuhudia moshi mweupe ukifuka huku kengele zikigongwa wakati wa tukio hilo kuashiria kuwa makardinali 133 wamemchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani.

Leo wa XIV anakuwa Papa wa 267 toka kanisa katoliki lilipoanza kumhesabia Mtume Petro kama Papa wa kwanza

Papa Leo wa XIV aliyekua kiongozi wa Dikasteri ya Maaskofu na Rais wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini tangu mwaka 2023. Kabla ya hapo alihudumu kama Askofu wa Chiclayo nchini Peru kutoka 2015 hadi 2023.

Hata hivyi kabla ya kuwa Askofu wa Chiclayo alikuwa mkuu wa shirika la Mtakatifu Agustino (OSA) kutoka mwaka 2001 hadi 2013.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents