Habari

Kiongozi wa zamani wa China, Jiang Zemin afariki dunia

Kiongozi wa zamani wa China, Jiang Zemin afariki dunia

Rais wa zamani wa China, Jiang Zemin amefariki dunia leo siku ya Jumatano Novemba 30, 2022 akiwa na umri wa miaka 96.

Vyombo vya habari nchini China vimeripoti kuwa, Jiang Zemin amefariki dunia Novemba 30, 2022 kutokana na saratani na kufeli kwa baadhi ya viungo vya miwili.

Jiang Zemin amezaliwa Jiangsu Agosti 17, 1926 amewahi kuwa katibu mkuu wa chama cha Chinese Communist Party kuanzia June 1989 hadi Novemba 2002 na kufanikiwa kuiongoza China kuanzia mwaka 1993 hadi 2003.

Jiang hakuonekana kwenye mikutano ya hadhara tangu mwaka 2019 huku taarifa juu ya afya yake ilianza kuenea baada ya kukosekana kwenye mkutano wa chama chake mwaka 2021.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents