FahamuHabariSiasa

Kiongozi wa zamani wa Hamas aunga mkono mashambuzi Israel

Kiongozi wa zamani wa Hamas amesema walichokifanya wanamgambo hao Jumamosi iliyopita ni “jaribio la kumaliza uvamizi wa Israel” na kwamba “anajivunia” waliotekeleza shambulio hilo

Akizungumza na Haberturk TV ya Uturuki, mkuu wa masuala ya kigeni wa Hamas Khalid Meshal aliongeza mzozo huo haukuanza wiki iliyopita, bali mwaka 1948.

“Israel imekuwa ikisema kuwa jeshi lao lilikuwa na nguvu zaidi na lisiloweza kushindwa. Tulipoona kwamba wameshindwa kwa saa chache, tulishangaa pia,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu mashambulizi ya wanamgambo wa Hamas dhidi ya raia, watoto na wazee, alisema: “Tuliendelea kuwaambia wasifanye hivyo. Lakini nyakati za vita, matukio haya yanaweza kutokea. Je, si ndivyo Israel inavyosema kila mara, kwamba wao hawakufanya hivyo [kuwaua raia] kwa makusudi?”

Alipoulizwa kama Hamas imefanya sawa na inavyoishutumu Israeli kufanya, Meshal alisema kulikuwa na “tofauti kubwa”:

“Sisi ndio wamiliki wa ardhi hii. Adui anapotoka nje, ama askari au raia, wote ni maadui. Yeyote anayekuja katika ardhi yangu [kuikalia] ni adui, na ana hatia.”

Marekani na China zazungumza kuhusu Israel-Gaza kwa njia ya simu

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametumia simu na mwenzake wa China Wang Yi kuomba msaada wa Bejing katika kuhakikisha mzozo wa Israel na Hamas hauenei katika nchi nyingine za Mashariki ya Kati.

Kwa upande wake, Wang alisema Washington inapaswa “kuchukua jukumu la kujenga na kuwajibika”:

“Wakati wa kushughulika na masuala ya kimataifa, nchi kubwa lazima zifuate usawa , kudumisha utulivu na kujizuia, na kuongoza katika kutii sheria za kimataifa,” alisema Wang.

Waziri wa mambo ya nje wa China pia ameongeza kuwa Beijing imetoa wito wa “mkutano wa kimataifa wa amani” haraka iwezekanavyo.

Taarifa rasmi za China kuhusu mzozo huo hazijawataja haswa Hamas katika kulaani ghasia, badala yake zimehimiza kusitishwa mara moja kwa mapigano, kulaani “matumizi ya nguvu kiholela”, na kutaka kukomeshwa kwa “adhabu ya pamoja ya watu huko Gaza”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents