HabariMichezo

Kipaumbele changu ni ushindi- Robertinho

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema ataingia katika mchezo wa leo Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji kwa lengo la kutafuta ushindi ili kupunguza tofauti ya alama walizoachwa na Yanga SC.

Robertinho ameongeza kuwa Simba ni timu kubwa na malengo yake ni kushinda ubingwa hivyo kila mchezo wanahitaji kupata alama tatu.

“Tuna nafasi ya kuonyesha Simba ni timu kubwa. Baada ya kambi ya wiki moja Dubai kufanikiwa tunahitaji kushinda na kuonyesha soka safi. Ili kuwa bingwa lazima kuchukua alama tatu,” amesema Robertinho.

Nyota watatu ambao wamewasajili mwishoni mwa dirisha kiungo Ismael Sawadogo na washambuliaji Jean Baleke na Mohamed Mussa ni miongoni mwa wachezaji 19 waliosafiri nao kwenda Dodoma kwa ajili ya mchezo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents