AfyaHabari

Kipindupindu DRC, watu 256 walazwa

Wafanyakazi wa misaada Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alhamisi wameonya kuhusu janga la afya kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi ya kipindupindu kwenye kambi za muda za wakimbizi.

Madkatari wasio na mipaka maarufu MSF wamesema kwamba kati ya Novemba 26 na Desemba 7, wagonjwa 256 wamelazwa kwenye kituo chao cha afya kilichoko Munigi karibu na mji wa Mashariki mwa Goma.

MSF wameongeza kusema kwamba theluthi moja ya wagonjwa waliofikishwa kituoni humo ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Zaidi ya watu 177,000 sasa hivi wamekwama kwenye kambi za wakimbizi katika hali hatarishi, baada ya kukimbia mashambulizi kutoka kundi la M23 katika wiki za karibuni.

MSF limeongeza kusema kwamba idadi ya maambukizi mapya ya kipindupindu katika siku 10 zilizopita yameongezeka maradufu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents