Michezo

Kiswahili cha Kim Poulsen chaimarika, azungumzia Stars Vs Madagascar (+Video)

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania raia wa Denmark, Kim Poulsen hii leo amezungumzia mchezo dhidi ya Madagascar utakaopigwa hapo kesho Jumanne Septemba 7, 2021 Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Kama kawaida yake, Kim Poulsen ameanza mkutano wake na wanahabari kwa kutumia lugha adhimu ya Kiswahili huku akionekana kuwa na kiu ya kuifahamu vizuri mno na haya yakiwa baadhi ya maongezi yake kwa Kiswahili ”Habari za asubuhi, kidogokidogo.” Juma lililopita wakati akitangaza kikosi cha timu ya Taifa, Kim Poulsen alisema kuwa anataka kufanya mazoezi kwa lugha ya Kiswahili na ndipo akatangaza kikosi ”Nataka kutangaza kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars,” maneno aliyozungumza kabla ya mchezo dhidi ya DR Congo ambao Stars walifanikiwa kuondoka na alama moja muhimu wakiwa ugenini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents