Habari

Kitongoji chafungwa kusaka waalifu El Salvador

Serikali ya El Salvador imewaamuru wanajeshi 10,000 na maafisa wa polisi kuzingira kitongoji kimoja katika mji mkuu wa nchi hiyo, San Salvador unaojulikana kuwa ngome ya magenge ya wahalifu.

Picha zilizotolewa na serikali zilionyesha wanajeshi wakiwa wamevalia fulana za kuzuia risasi huku wakiwa na silaha nzito.

Rais Nayib Bukele, amekuwa akipambana kuyamaliza magenge ya wahalifu kwa miezi tisa amesema serikali yake inalenga kupunguza matukio ya mauaji.

Magenge hayo yamekuwa mashuhuri kwa kupora pesa kutoka kwa wafanyabiashara na yamedhiti maeneo mengi ya mji mkuu wa taifa hilo.

Barabara za kuingia na kutoka katika kitongoji cha Soyapango zilifungwa ili maaafisa waendeshe zoezi la kukagua vitambulisho vya watu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents