Technology

Kituo kikubwa cha Google Afrika kitakuwa Nairobi

Kampuni ya Google Alphabet Inc (GOOGL.O) inawekeza katika kituo chake cha kwanza cha ukuzaji wa bidhaa barani Afrika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Mnamo mwaka wa 2018 kampuni hiyo ilitangaza mpango wa uwekezaji wa $1bn (£770m) kwa Afrika kufaidika na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa mtandao katika bara hilo.

“Kufikia 2030, Afrika itakuwa na watumiaji milioni 800 wa mtandao … na Google imejitolea kuharakisha mabadiliko ya kidijitali barani Afrika kupitia kuwezesha mtaji wa watu,” Nitin Gajria, Mkurugenzi Mkuu wa Google barani Afrika alisema.

Mapema mwaka huu, kampuni ya teknolojia ya malipo ya Visa na kampuni kubwa ya programu za kompyuta ya Microsoft pia ilifungua vituo vya uvumbuzi jijini Nairobi.

Vituo hivyo vitakuwa na nafasi za kazi kwa wahandisi wa programu, watafiti na wabunifu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents