Siasa

Kiwango kipya cha kikokotoo chatangazwa 

Serikali imetangaza kiwango kipya cha kikotoo cha mafao ya mkupuo ambapo sasa ni asilimia 33 kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii.

Tangazo hilo la Serikali limeyolewa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu Profesa Jamal Katundu.

Amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano kati ya Serikali, Chama cha Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) baada ya kusitishwa kwa kanuni zilizotengenezwa mwaka 2018.

Profesa Katundu amesema wamekubaliana kikokotoo limbikizi kitakuwa 1/580.

Amesema mshahara wa kukotolea mafao ya pensheni utakuwa wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu.

Related Articles

Back to top button