Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMahojiano

Kizz Daniel afunguka mwanzo mwisho sababu za kutokufanya Show

Msanii wa muziki kutoka nchi Nigeria amezungumza na wana habari leo katika hotel ya Rotana na kuomba msamaha. Mbali ya kuomba msamaha msanii huyo amesema atarudia show yake siku ya Ijumaa. Waandaaji wa Show hiyo qameeleza kuwa watataja sehemu ambapo show hiyo itafanyika.

“Nilipofika Nairobi toka Kampala ndege niliyotakiwa kuunganisha nayo nilikuta imeshaondoka, nilikaa Nairobi kwa masaa nane, nikapata ndege ya kuunganisha saa mbili na nusu usiku. Nilipofika Dar tukagundua kuna vitu vyangu vimesahaulika, wakasema watanitumia”

“Hata hivyo nilikaa na promota na wandaaji tukakubaliana kwamba tufanye kitu kwa ajili ya mashabiki na tukakubaliana kwamba show lazima iendelee, itafanyika Ijumaa wiki hii. Naomba radhi kwa mashabiki, sikukusudia kufanya hivi, sikuwa na lengo la kuwaudhi”

“Naipenda kazi yangu, nilikuja kutumbuiza na ninakusudia kutumbuiza. Ni matumaini yangu kwamba mtanipa nafasi nyingine ya kutumbuiza Ijumaa – Kizz Daniel

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents