HabariMichezo

Klabu inayomtaka Morrison ituandikie barua – CEO Barbara

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amedai kuwa Bernard Morrison hakuwa kwenye mipango yao hasa kutokana na ripoti zake kujirudia rudia.

“Tulimpa Morison barua ili apate nafasi ya kutafuta timu, hakuwa kwenye mipango yetu tena kutokana na ripoti zake kujirudia rudia hasa zile za nje ya uwanja. Hata yeye alijua Simba hakuna nafasi ya kuongeza mkataba tena,” Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amedai kuwa

Barbara amesema kuwa Klabu inayomtaka Morrison ndiyo inayopaswa kuandika barua na sio mchezaji ameyasema hayo kupitia Tv3.

”Mchezaji anaomba aondoke kabla ya mkataba, na kama anataka kuondoka kabla ya mkataba lazima aombe kwa maandishi na sisi tulimuomba yeye hawezi kuandika ila Klabu inayomtaka lazima iandike mfano Amazulu ilituandikia kwamba tunamuhitaji Rally Bwaliya, nimemwambia Morrison mimi sina shida waambie watuandikie, andika mimi nitajibu, kwa nini ile klabu inagoma kutuandikia ?.”- CEO Barbara Gonzalez.

Imeandikwa na Hmaza Fumo, Instagram @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents