Klabu sita zaingi katika vita kubwa ya kutaka kumsajili mchezaji hatari wa Manchester City

Everton imejiunga na Chelsea, Leeds United, Tottenham, Barcelona na Inter Milan ambao wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, ambaye atapatikana kwa uhamisho huru atakapoondoka Manchester City msimu wa joto. (Daily Star on Sunday)

Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah amesema Liverpool haijazungumza naye kuhusu kuongeza mkataba wake na klabu hiyo, huku mkataba wake ukitarajiwa kumalizika mwaka 2023. (Sky Sports)

Arsenal wanaamini wanaweza kumchukua kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma kwa kitita cha pauni milioni 30 (Daily Star on Sunday)Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah amesema Liverpool haijazungumza naye kuhusu kuongeza mkataba wake

Mlinzi wa klabu ya Uhispania Sergio Ramos, 35, bado ana matumaini ya kuongezewa mkataba wa miaka miwili na Real Madrid, ambao wamempa ofa ya mwaka mmoja pekee. (Marca)

Manchester United itamuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba msimu huu wa joto ikiwa mchezaji huyo mwenye miaka 28 kama hatakubali kusaini kataba mpya.(Sun on Sunday)Mlinzi wa klabu ya Uhispania Sergio Ramos ana matumaini ya kusalia Real Madrid

Mkataba wa mlinda mlango Muitaliano Gianluigi Dinnarumma na AC Milan unakwisha msimu wa joto na wakala wake, Mino Raiola, amefanya mazungumzo na Juventus kuhusu mchezaji huyo mwenye miaka 22 kujiunga nao (Calciomercato-in Italian)

AC Milan wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 23, ambaye pia ananyemelewa na West Ham. (Standard)

Kocha anayeondoka wa Bayern Munich Hansi Flick anataka kuwa kocha wa Ujerumani, Joachim Low atakapoondoka baada ya msimu wa joto wa ligi ya mabingwa Ulaya na hana mpango wa kwenda Tottenham. (Sport1-in Germani)Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham,

Kocha wa Fulham Scott Parker pia anaibuka kuwa mmoja wa makocha ambao huenda wakachukua nafasi ya Jose Mourinho aliyetimuliwa Tottenham, klabu ambayo Parker aliichezea kwa miaka miwili. (Football Insider)

Tottenham imejiunga kwenye kinyang’anyiro cha kujaribu kupata saini ya mshambuliaji wa Brentford, Muingereza Ivan Toney, 25. (Football Insider)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta atakuwa tayari kumpa nafasi kiungo wa kati Muingereza Joe Willock, anayecheza kwa mkopo Newcastle United, ndani ya kikosi cha washika bunduki. (Shiellds Gazzette)

Mshambuliaji wa Brentford, Muingereza Ivan Toney

Arteta pia amesema Arsenal ”watakuwa na mazungumzo kuhusu hilo” watakapofikia hatua ya kuongeza mkataba wa kiungo wa kati Emile Smith Rowe, 20. (Sky Sports)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Mhispania Eric Garcia yuko mbioni kuridhia mkataba ambao utamfanya kujiunga na Barcelona kwa uhamisho huru mkataba wake na Manchester City utakapokwisha majira ya joto. (Mundo Deportivo)

Related Articles

Back to top button