Klabu ya Manchester City imeondoa bidha zote zenye jina la Benjamin Mendy baada ya kushitakiwa kwa ubakaji (+ Video)

Klabu ya Manchester City imeondoa bidhaa zote zinazohusiana na Benjamin Mendy kutoka kwa wavuti yake rasmi na duka la mkondoni kufuatia mashtaka ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia wa mlinzi wa Ufaransa.

Imeelezwa kuwa Mendy, 27, ataachwa na klabu hiyo mwezi Januari baada ya kushtakiwa kwa makosa manne ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kijinsia mwezi uliopita.

Beki huyo wa kushoto alionekana katika Korti ya Chester Crown mnamo Ijumaa iliyopita na aliwekwa rumande na Kutakuwa na usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo mnamo Novemba 15 wakati Mendy na mshtakiwa mwenzake Louis Saha Matturie, wa Eccles, ambaye pia ameshtakiwa kwa makosa manne ya ubakaji, watakapotoa maombi yao.

Tarehe ya kesi imewekwa Januari 24 mwaka ujao na inatarajiwa kudumu kwa wiki mbili hadi tatu.

Mendy alisimamishwa kazi na City baada ya kushtakiwa na polisi na sasa haiwezekani tena kuagiza jezi ya Man City yenye jina na nambari yake kupitia tovuti rasmi ya kilabu au duka la mkondoni.

Ingawa Taarifa zote za mchezaji huyo bado zinapatikana kwenye tovuti ya klabu ingawa inafanya iwe wazi kuwa Mendy kwa sasa amesimamishwa, lakini pia haiwezekani tena kutafuta bidhaa zake zozote.

Katika taarifa iliyotolewa mwezi uliopita, kilabu ilisema: “Manchester City inaweza kuthibitisha kwamba baada ya kushtakiwa na polisi leo, Benjamin Mendy amesimamishwa kazi kusubiri uchunguzi.

Bofya hapa chini kutazama.

 

https://www.instagram.com/p/CTy4VcDDYr0/

Related Articles

Back to top button