Habari

Kliniki ya kwanza ya kisasa ya meno yazinduliwa Dar

KLINIKI ya kwanza ya kisasa ya meno na kinywa imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam ili kutoa suluhisho la kudumu la matatizo ya meno nchini.

CEO wa Afya Bora Complete Dentistry Clinic Mrs. Donna-Williams Ngirwa, DDS akiwa na ambassador wa clinic hiyo ya afya kamili ya kinywa Mwanamuziki Grace Matata katika uzinduzi wa Kituo hicho kilichopo Mikocheni Regent Street Block No. 7

Kliiniki hiyo ya kipekee inayojulikana kama AFYA BORA COMPLETE DENTISTRY LTD inalenga kuimarisha huduma za kinga ya meno. Hiki kitakuwa kituo cha kwanza kabisa kutoa huduma ya aina hii kikamilifu.

Mtendaji Mkuuu wa Kliniki hiyo, Dk. Donna Williams Ngirwa anasema kituo hki kitajikita zaidi katika kueneza elimu kuhusu uhusiano uliopo kati ya afya ya kinywa na afya ya binadamu kwa ujumla.
“Utafiti unaonyesha kuwa magonjwa mengi yakiwemo shambulio la moyo, kisukari, kiharusi, maambukizi katika mapafu na magonjwa mengine yana mahusiano ya karibu na maambukizi yaliyopo katika kinywa,” anasisitiza na kuongeza kuwa elimu hii nimuhimu iwafikie wananchi.

Dk. Williams Ngirwa amekuwa akishughulika na huduma za meno jijini Mwanza tangu akiwa mdogo na pia ana ofisi inayotoa huduma za afya ya meno nchini Marekani.
Aliwahi kuishi Mwanza mwanzoni mwa miaka ya 1970 na kujifunza mambo mengi kuhusiana na huduma hii jambo ambalo lilimshawishi kuanzisha huduma hii yeye na mume wake.
Kwa mujibu wa Dk. Gilbert Tarimo ambaye ndiye daktari bingwa katika kituo cha huduma ya meno na kinywa cha Afya Bora, lengo ni kuifanya huduma ya afya ya kinywa kuwa ya kinga zaidi badala ya tiba.

“Tunafanya uchunguzi wa afya ya kinywa na mgonjwa anapewa ripoti ya kila kitu kuhusu kinywa chake na hatua anazopaswa kuchukua ili kuboresha afya yake zaidi,” anasema
Dk. Williams Ngirwa anasema watu wengi wanaishi vizuri kwa kula chakula kizuri na kufanya mazoezi lakini wanakosa afya ya kinywa, pengo ambalo Afya Bora ya Kinywa wanaamua kuliziba.

Kituo hicho kilichoko mtaa wa Regent Estate jijini Dar es Salaam kinatoa huduma zote za meno ikiwemo usafishaji wa meno, kuweka meno ya bandia, mpangilio wa meno na huduma nyinginezo za tiba ya meno.
Dk. Williams Ngirwa anasema watatoa fursa kwa wahitimu wa elimu ya juu kikiwemo Chuo Kikuu cha Afya ya Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) kujifunza na kuimarisha fani ya udaktari wa meno.

Vilevile tangu mwezi Januari mwaka huu watoa huduma ya tiba ya meno wa hapa nchini wamekuwa wakishiriki mafunzo kuwawezesha kutoa huduma za kipekee na kuwawezesha madaktari bingwa wa meno ambao hawawezi kumudu kuanzisha kliniki zao binafsi, kufanya kazi katika kituo hicho.
Dk. Williams-Ngirwa amesema kwa vile watu hawana bima ya meno, mpango wa Afya Bora ya Meno utatoa huduma bure za uchunguzi wa meno, usafishaji wa meno, vipimo vya x-ray, na punguzo la asilimia 20 kwa tiba kamili ya meno.

Lengo kuu la Afya Bora ya Meno na Kinywa ni kuwajenga wananchi wawe na utamaduni wa kuthamini afya ya meno na kinywa ili kuboresha maisha yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents