Kocha aliyemsajili Samatta Aston Villa Dean Smith, atambulishwa Norwich City

Norwich City imemthibitisha Dean Smith kama kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili na nusu. Kocha huyo wa zamani wa Aston Villa, 50, anarithi mikoba ya Daniel Farke, ambaye alitimuliwa na Canaries wakiwa mkiani mwa Ligi ya Premia, pointi tano chini ya eneo salama katika jedwali .

Craig Shakespeare, ambaye alifanya kazi na Smith katika Villa Park, ataungana naye kama msaidizi wake huko Carrow Road.

“Kimekuwa kipindi kigumu cha siku saba,” alisema Smith, ambaye alifukuzwa na Villa mnamo 7 Novemba.

“Nimefurahi sana kurejea na kufanya kazi kwa Norwich City kwenye Ligi ya Premia.

“Ni wazi, kumekuwa na kazi nzuri ambayo imefanyika katika klabu hii ya soka katika kipindi cha miaka minne na nusu iliyopita. Sasa ni kazi yangu na Craig kuendelea na kuboresha kazi hiyo kwa lengo kuu la kusalia katika Premier. Ligi.”

Mchezo wa kwanza wa Smith utakuwa nyumbani dhidi ya Southampton tarehe 20 Novemba.

Ataweka historia ya kuwa mtu wa kwanza kuchukua usukani wa mechi mfululizo za Ligi Kuu dhidi ya mpinzani mmoja akiwa na timu tofauti, baada ya kutimuliwa na Villa kufuatia kushindwa na Saints.

Related Articles

Back to top button