Michezo
Kocha Julio ala shavu

Klabu ya Singida Fountain Gate imemtambulisha Jamhuri Kiwelu (Julio) kuwa kocha mkuu wa Klabu hiyo hadi mwisho wa msimu baada ya wiki nzima iliyopita kuvunja benchi zima la ufundi lililokuwa chini ya Kocha Thabo Senong.
Singida Fountain Gate imeamua kumpa time Julio baada ya kutoridhishwa na matokeo ya timu yao ilipokuwa chini ya Kocha Senong.
Kwasasa Singida Fountain Gate inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara baada ya kutuna pointi 21, wakiwa point 28 nyuma ya Yanga kinara wa Ligi hiyo.
Time hiyo imebakisha michezo 10 tu ili kuamua hatima yao katika ligi kuu au itaporomoka kwenda Championship msimu ujao.
Imeandikwa na Mbanga B.