
Imeripotiwa kuwa Klabu ya Paris Saint-Germain haina mpango wa kumtimua Kocha wake, Christophe Galtier licha ya kutolewa UEFA Champions League.
Hata hivyo, Galtier amepoteza ushawishi ndani ya ya kikosi cha PSG.
Mambo yalianza kumuendea mrama mara baada ya kupoteza mbele ya Bayern Munich in kwenye Michuano ya Champions League Jumatano usiku.
PSG imejaa mastaa kama Messi, Neymar, Mbappe na wengine wengi lakini chini ya Kocha, Galtier imeshindwa kutimiza ndoto za Ubingwa wa Champions League.
Imeandikwa na @fumo255