Michezo

Kocha wa Simba SC  amtimua Ibrahim Ajibu ”Ajibu aige mfano wa Manula” (+Video)

Kocha wa klabu ya Simba Mbelgiji, Sven Vandenbroeck amezungumzia hali ya mazoezi inavyoendelea ikiwa leo yamefikia siku ya tatu baada ya kuwa mapumziko kutokana na kusimama kwa ligi ili kuepusha kusambaa kwa Corona.

Akizungumzia baada ya mazoezi hayo, Sven Vandenbroeck amesema nyota wake Ibrahim Ajibu amemrudisha nyumbani baada ya kuchelewa kuingia kambini kwaajili ya mazoezi siku ya kwanza na hivyo kuungana na timu siku ya Jumatatu huku Mbelgiji huyo aliyerithi mikoba ya Patrick Aussems amewataja baadhi ya nyota wake ambao wameshindwa kuungana na timu mpaka sasa kutokana na nchi zao kuwa katika ‘Lockdown’ ya Corona kuwa ni Mzambia, Clatous Chama, Francis Kahata kutoka nchini Kenya pamoja na Msudani, Sharaf Eldin Shiboub.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents