HabariMichezo

Kocha wa Taifa Stars afungiwa michezo 8, Mgunda na Morocco warithi mikoba

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemfungia mechi nane Kocha wa timu ya Taifa (Taifa
Stars), Adel Amrouche.

Adhabu hiyo ilitolewa jana na Kamati ya Nidhamu ya CAF, malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (RMFF) dhidi ya Kocha Amrouche.

RMFF ilimlalamikia Kocha huyo kwa kauli zake kuwa Morocco inaushawishi ndani ya CAF katika kupanga mechi pamoja na waamuzi.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemsimamisha Kocha Adel Amrouche.

Kutokana na uamuzi huo, imemteua Hemed Morocco kuwa Kaim Kocha, na atasaidiwa na Juma Mgunda.

Tumaini lako lipoje AFCON kupitia kwa makocha wazawa?? JUMA MGUNDA NA HEMED MOROCCO??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents