Afya

Louis van Gaal aweka wazi kusumbuliwa na saratani

Meneja wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal anasema anapokea matibabu ya saratani ya tezi dume. Mholanzi huyo ambaye kwa sasa anaiongoza timu ya taifa ya Uholanzi, alitoa tangazo hilo kwenye kipindi cha televisheni cha Uholanzi Humberto siku ya Jumapili.

Van Gaal, 70, alisema ameficha habari hizo kutoka kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya hivi majuzi ya kimataifa.

“Sikutaka kuwaambia wachezaji wangu kwa sababu ingeweza kuathiri uchezaji wao,” aliongeza.

Van Gaal yuko katika kipindi chake cha tatu kama kocha mkuu wa Uholanzi, akiwa ameiongoza hadi nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia la 2014 na sasa kwenye fainali za 2022 huko Qatar.

Aliongeza: “Katika kila kipindi nikiwa meneja wa timu ya Taifa nililazimika kuondoka usiku kwenda hospitali bila wachezaji kujua mpaka sasa, huku nikidhani ni mzima wa afya, lakini.. sipo. “

Katika kipindi cha miaka miwili akiwa Manchester United, Van Gaal aliiongoza kufanikiwa Kombe la FA mnamo 2016 kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.

Pia ameshinda mataji ya ligi akiwa na Barcelona, ​​Bayern Munich, AZ Alkmaar na Ajax, ambapo aliiongoza timu hiyo ya Uholanzi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka 1995.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents