Koimizo Abdul Abass MAÏGA namba 6 mpya Yanga

YANGA inafanya mambo yake ya usajili kimyakimya kwa ajili ya msimu ujao, hiyo ni baada ya kujihakikishia mapema tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kwa sasa kuongoza msimamo wa ligi na mapema tu imeanza kuboresha kikosi chake. . Chanzo changu cha kuamjnika kutoka ndani ya Yanga kimeniambia Viongozi wameanza kufabya mazungumzo na kiungo Mkabaji wa Asec Mimosa, Koimizo anayecheza eneo la kiungo mkabaji, anatarajiwa kwenda kuchukua nafasi ya Khalid Aucho. .
Kwa mujibu ya mkataba wa Aucho ambao aliongeza mwaka mmoja msimu uliopita, mwisho wa msimu huu unamalizika na haijafahamika kama kuna mazungumzo yoyote kwa pande zote mbili huku taarifa zikibainisha hatakuwa na kikosi hicho msimu ujao. .
“Hakuna mchezaji mbaya ambaye tumemtoa Asec Mimosas, ukiangalia ni timu yenye vipaji vikubwa, si unaona Pacome (Zouzoua), Aziz Ki (Stephane) na Yao (Kouassi Attohoula), hivyo ni suala la muda tu kumalizana naye na kila mmoja atamuimba. Kiungo mkabaji tangu ametua Aucho ambaye analituliza eneo hilo akicheza kwa ubora tumekuwa tukibahatisha kupata mchezaji mwingine bora wa kumpa changamoto, lakini kwa huyu wa Asec tunaamini ataleta kitu cha tofauti.” . Kiungo huyo ni zao la Saint-Etienne ya Ufaransa, kama akitua Yanga atakuwa ni mchezaji wa nne kutoka Asec baada ya Stephane Aziz Ki, Yao Kouassi Attohoula na Pacome Zouzoua