Kongamano la Biashara na uwekezaji la Ziwa Tanganyika laleta neema Kigoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amezindua rasmi Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Ziwa Tanganyika lililofanyika katika Hoteli ya Lake Tanganyika, mkoani Kigoma.
Kongamano hili linalenga kuimarisha nafasi ya Kigoma kama kitovu cha biashara na uwekezaji katika ukanda wa Maziwa Makuu. Linalenga kuvutia wawekezaji, kuchochea ajira, na kukuza ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na nchi jirani zilizopo kwenye Ushoroba wa Kati.
Serikali inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kufungua fursa za kiuchumi kupitia uboreshaji wa miundombinu na mazingira wezeshi ya biashara kwa manufaa ya wananchi wa Kigoma na Taifa kwa ujumla.
Kongamano hili la siku mbili ambalo linaenda sambamba na maonesho ya siku nne, limeandaliwa na kuratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TanTrade, chini ya Mkurugenzi Mkuu Dkt. Latifa Mohamed Khamis, ambapo moja ya majukumu ya Mamlaka hii kisheria ya kukuza biashara, kutanua masoko, na kuunganisha wazalishaji wa Tanzania na wawekezaji wa kikanda na kimataifa.
Written by Janeth Jovin







